MATAPO YA NYIMBO ZA SHISAFWA

Pendo Mwashota, Fokas Nchimbi

Abstract


Makala haya yanalenga kuibua mabadiliko mbalimbali yanayojitokeza katika nyimbo za jamii ya Kisafwa. Mabadiliko yanayoelezwa katika makala haya yamegawanyika katika sehemu kuu mbili. Mabadiliko ya kimaudhui na mabadiliko ya kifani. Katika suala la maudhui, makala yanaeleza kuwa kuna mabadiliko kwa kiasi fulani katika nyimbo za jamii ya Shisafwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali kwani watunzi na waimbaji wengi wa sasa wanaelekea kujali zaidi soko na sio ujumbe unaotakiwa kuifikia jamii. Aidha, mabadiliko katika fani yamejitokeza katika vipengele tofautitofauti kama vile uwasilishaji, ushiriki, vifaa, hadhira na madhari. Hali hii inaonesha namna mwingiliano wa kijamii unavyoelekea kuwa na athari katika mambo mbalimbali yanayowazunguka wanajamii husika mpaka katika fasihi yao. Pengine ni kutokana na uhai wa kazi za fasihi yaani kutokuwa tuli kwa sababu kadri jamii inavyobadilika ndivyo na taratibu na mambo mengine yanayoizunguka yanavyobadilika.

 


Full Text:

pdf

Refbacks

  • There are currently no refbacks.