Uchambuzi wa Toni kwa Mkabala wa Kiinitoni na Tonijuu Msingi: Uchunguzi wa Lugha ya ki-Meetto -Makuwa cha Tanzania

Joseph Hokororo Ismail

Abstract


Kumekuwa na taratibu mbalimbali za toni zinazotumika katika uibuzi wa umbo la nje kutoka umbo la ndani. Wataalamu wa fonolojia walioshughulikia toni, mathalani Goldsmith (1976) na Massamba (1982), wamechanganua toni kwa kutumia mkabala uliozingatia matumizi ya kiinitoni ambacho huchombeza utokeaji wa toni; wakati wataalamu wengine kama vile Odden (1989), Batibo (1990), Robert (1992), Matondo (2003) na Marlo (2007) wamechambua toni kwa kutumia mkabala unaozingatia tonijuu msingi kama chanzo cha uibuzi huo. Hawa wa kundi la pili wanaona kwamba kanuni mbalimbali zinazofuatia uibuzi huo huchimbuka kutoka katika tonijuu msingi hiyo. Lengo la makala hii ni kuzungumzia jinsi lugha ya ki-Meetto-Makuwa iliyochanganuliwa kwa misingi ya kiinitoni kuchombeza utokeaji wa toni, inavyoweza kuchambuliwa kwa mkabala unaozingatia tonijuu msingi kama Msingi wa uibuzi. Ingawa mikabala yote ipo katika Nadharia ya Fonolojia Vipandesauti Huru kama ilivyoasisiwa na Goldsmith (1976), lakini uchambuzi wa toni kwa mkabala wa tonijuu msingi, licha ya kuleta uwazi zaidi, unapunguza pia idadi ya kanuni zinazotumika katika uibuzi huo wa toni na kusaidia kuwa na kanuni chache katika uibuzi wa toni katika ki-Meetto-Makuwa na lugha nyingine za Kibantu.


Full Text:

pdf

Refbacks

  • There are currently no refbacks.