Dhana ya Zubu katika Nyimbo za Harusi za Waswahili: Uchambuzi wa Kisaikolojia Changanuzi

Issa Mwamzandi

Abstract


Zubu (au dhakari, uume) kama sehemu ya mwili wa mwanamume hufahamika kama kiungo cha kuendeleza uzazi. Pamoja na fasili hiyo, makala haya yanachukua mtazamo wa kisaikolojia changanuzi unaotazama zubu sio tu kama kiungo cha kibiolojia bali kinachoweza kuwa na viashiria mbalimbali na vyenye athari tofautitofauti. Kupitia nyimbo za harusi za Waswahili, neno zubu linabainika kama mdokezo wa maisha ya ndoa na mahusiano yanayotarajiwa na wanajamii baina ya jinsi ya kike na ya kiume. Makala yanabainisha kwamba kuwa na zubu (na vilevile kutokuwa nalo) ni njia ya kufafanua mahusiano ya yule mwenye mamlaka na, vilevile, asiyekuwa nayo katika jamii ya Waswahili. Kwa utaratibu huo, zubu limebeba viashiria muhimu vya kuwafunza maarusi namna wanavyopaswa kuishi, wao wenyewe kwanza, na kisha namna wanavyostahili kutangamana na wanajamii wengine. Mbali na kuzungumzia mahusiano ya kijinsi, viashiria vinginevyo vya saikolojia changanuzi vya woga, na ambavyo vinaendelezwa na dhana ya zubu, pia vimefafanuliwa na makala.

Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.