Mtindo katika Hotuba za Rais J.P. Magufuli na Mchango wake katika Maendeleo ya Lugha ya Kiswahili

Ahmad Y. Sovu

Abstract


Baada ya Mheshimiwa J.P. Magufuli kutawazwa kuwa Rais wa Tanzania, shughuli zake rasmi za kila siku zilihusisha matumizi ya Kiswahili. Makala yanaeleza: (i) Vibainishi vya mitindo ya lugha ya kisiasa anavyovitumia katika hotuba zake (ii) Ikiwa matumizi ya lugha katika hotuba yana mchango katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili. Makala yanadhihirisha kuwa katika hotuba hizo Rais Magufuli hutumia vibainishi vifuatavyo: istilahi maalumu, nafsi ya kwanza wingi na umoja, misemo, uradidi wa maneno, lugha ya matumaini, takwimu, balagha, mzaha, lugha yenye mshikamano na lafudhi za lugha za makabila. Makala inabaini mchango wake katika maendeleo ya Kiswahili kuwa ni: Kukuza fasihi ya Kiswahili, kukuza msamiati wa Kiswahili, kuongeza fursa za ajira kwa wataalamu wa Kiswahili, kuwatia ari wakalimani, wafasiri na pia kuwahimiza wananchi katika kuthamini matumizi ya lugha ya Kiswahili. Makala inatoa mchango mkubwa katika uga wa lugha ya siasa kwa kudhihirisha namna vipengele anuwai vya lugha ya kisiasa vinavyotumika katika hotuba za viongozi wa kisiasa na taathira yake katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili.

Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.