Tungo za Mrisho Mpoto: Sitiari ya Mwenendo wa Siasa na Utawala Nchini

Manyuka Majuto Kapaya

Abstract


Mrisho Mpoto ni mwanamuziki anayetumia mtindo wa kughani mashairi na kuimba nyimbo zenye mahadhi ya Kiafrika. Moja ya mambo yanayoupa upekee ushairi wake ni matumizi ya lugha fasaha na sanifu ya Kiswahili iliyojaa utajiri wa mbinu mbalimbali za kisanaa zikiwamo tamathali za semi, methali, nahau, misemo na mafumbo. Matumizi ya mbinu za kisanaa hasa tamathali za semi na ujenzi wa sitiari ya jumla katika tungo za Mpoto yamefanya mashairi yake kuwa magumu na yasioeleweka kirahisi. Kazi zake nyingi zinashughulikia siasa, jambo ambalo ni sehemu ya maisha ya kila mtu. Ni kusudi la makala haya kuchunguza namna ambavyo msanii amejenga sitari kudurusu mwenendo wa siasa na utawala nchini Tanzania. Kumekuwa na upungufu wa kazi zinazohakiki nyimbo za wasanii wa muziki kutokana na ukweli kuwa wahakiki wengi hupenda kuhakiki diwani, riwaya na tamthiliya ambazo zipo katika maandishi. Katika makala haya tutachambua nyimbo tatu za Mpoto: ‘Njoo Uchukue’, ‘Sizonje’, na ‘Kitendawili’.

Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.