MULIKA ni jarida la taaluma ya Lugha na Fasihii ya Kiswahili. Lilianzishwa mwaka 1970. Jukumu lake kuu ni kukusanya na kusambaza maarifa yanayohusu Lugha na Fasihi ya Kiswahili yaliyokitwa katika utafiti mpevu. MULIKA limeendelea kuwa daraja kati ya watumiaji wa Kiswahili popote walipo, na wataalamu wa Kiswahili katika Sekondari na Vyuo vya Elimu ya Juu Afrika ya Mashariki.
Habari za Mkondoni
Jarida hili linapatikana pia mkondoni kupita tovuti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam www.udsm.ac.tz. Aidha, utaratibu wa kuingiza jarida hili katika tovuti ya majarida ya Afrika mkondoni AJOL uko ukingoni. Utaratibu huu utakapokamilika jarida hili litapatikana katika www.ajol.info.
KAMATI YA UHARIRI
Dkt. Ernesta Simon Mosha | - | Mkurungenzi, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili |
Prof. Mugyabuso M. Mulokozi | - | Mhariri Mkuu |
Dkt. Mussa Hans | - | Mhariri Msaidizi |
Dkt. Lutz Diegner | - | Chuo Kikuu cha Humboldt (Ujerumani) |
Dkt. Athumani Ponera | - | Chuo Kikuu cha Dodoma (Tanzania) |
Dkt. Miriam Kenyani Osore | - | Chuo Kikuu cha Kenyatta (Kenya) |
WASHAURI WA WAHARIRI
Prof. Cyprean Niyomugabo | - | Chuo Kikuu cha Rwanda (Rwanda) |
Prof. Sangai Mohochi | - | Chuo Kikuu cha Rongo (Kenya) |
Dkt. Abel Mreta | - | Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Tanzania) |
Dkt. Joseph Nyehita Maitaria | - | Chuo Kikuu cha Karatina (Kenya) |
Dkt. S.S. Sewangi | - | Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) |
Prof. Ipara Odeo | - | Chuo Kikuu cha Kibabii (Kenya) |
Dkt. Wael Nabil Ibrahim | - | Chuo Kikuu cha Al Azhar (Misri) |
ADA KWA MWAKA
Afrika Mashariki | - | Shilingi za Kitanzania 5,000 |
Kwingineko | - | Dola za Kimarekani 40 (kwa ndege) |
MAELEKEZO KWA WAANDISHI WA MAKALA
Jarida huchapishwa mara moja kwa mwaka.
Jarida linapokea Makala yaliyoandikwa kwa Kiswahili TU. Makala yapigwe chapa kwenye karatasi za A4, mistari ikitengwa kwa kipimo cha nafasi mbili. Upande mmoja tu wa karatasi utumiwe.
Mwandishi awasilishe kwa Mhariri, nakala tatu za muswada wake, pamoja na nakal tepe iliyowekwa katika mfumo wa kikompyuta katika muundo wa Microsoft WORD.
Ukurasa wa kwanza wa Makala uoneshe jina la Makala, jina kamili la mwandishi (au waandishi) wa Makala (Ikiwa ni pamoja na wadhifa wake) na anwani yake.
Ukurasa wa pili uoneshe jina la Makala na ufupisho wa Makala (Ikisiri) kwa maneno yasiyozidi 300. Jina la mwandishi lisiandikwe.
Unapotaja marejeleo kwenye matini taja jina la mwisho la mwandishi, likifuatiwa katika mabano na tarehe ya chapisho lake na kurasa zilizorejelewa, k.m. Yahya (1983:139). Kwenye orodha ya marejeleo au bibliografia majina ya marejelewa yapangwe kialfabeti.
Tanbihi ziwekwe namba na zitumike pale tu inapobidi. Maelezo ya tanbihi yatolewe kwenye ukurasa wa pekee mwisho wa Makala.
Makala yatatathiminiwa na walau wasomaji wawili, bila ya wao kujua mwandishi ni nani. Waandishi waepuke kuweka utambulisho wowote katika Makala zao ili wanaosoma Makala hayo na kuyatathmini wafanye kazi yao kwa uyakinifu. Waandishi ambao Makala yao yatakubaliwa kuchapishwa watapatiwa NAKALA MOJA YA Jarida lenye Makala yao pamoja na malopoo kumi ya Makala yao.
Makala yapelekwe kwa:
Mhariri
MULIKA,
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
S.L.P. 35110,
DAR ES SALAAM, Tanzania
Barua pepe: mulika1970@udsm.ac.tz; mulika.udsm@gmail.com; iks@udsm.ac.tz
Simu: +255222410343.
Maoni yaliyomo katika Jarida hili ni ya waandishi wa makala, na si lazima yakubaliane na yale ya Wahariri au Taasisi ya Taaluma za Kiswahili.