Usomaji wa Riwaya ya Fanani ya Zainab Baharoon kwa Kuzingatia Mawazo ya Mikhail Bakhtin

Authors

  • Kyallo W. Wamitila Chuo Kikuu cha Nairobi

Abstract

Makala haya yamechunguza riwaya ya Fanani iliyoandikwa na Zainab Alwi Baharoon kwa kuongozwa na misingi ya Nadharia ya Usemezano inayohusishwa na mhakiki wa Kirusi, Mikhail Mikhailovich Bakhtin. Msingi na kichocheo kikuu cha uchunguzi huu ni kuwapo kwa sifa ya kisemezano katika kiwango cha kijuujuu (au kwa maneno ya wananaratolojia paramatini, chochote kilicho nje ya matini kama blabu, utangulizi n.k.) kutokana na kuwapo na watunzi wawili katika ukurasa wa hakimiliki, mmoja wa nathari (Zainab Alwi Baharoon) na mwingine wa tungo za kishairi (Ali Saleh) zinazopatikana ndani ya kazi moja ya kifasihi. Katika makala haya tumejaribu kuendeleza mjadala wa usemezano huo katika kiwango hicho, kwa kuonesha ni kwa namna gani inawezekana kudai kuwapo kwa sauti anuwai katika riwaya yenyewe pamoja na dhana nyingine za nadharia hiyo kama utohitimishikivu, mgotanisho wa sauti na mtanziko wa kimaadili. Makala haya yameelekezwa kwenye uwezekano wa kifasiri na kiusomaji wa riwaya hii yanayoweza kukuzwa kwenye tahakiki za baadaye kuhusu riwaya hii na nyingine zenye sifa sawa nayo.

DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na44t1.1

  

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2025-06-30

Issue

Section

Articles