Habari za Mkondoni

Jarida hili linapatikana katika tovuti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa anwani https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj. Utaratibu wa kuingiza jarida hili katika tovuti ya majarida ya Afrika mkondoni (AJOL) unasubiri kukamilika kwa mchakato wa sekretarieti ya AJOL kwa mujibu wa kanuni na miongozo yao. Aidha, mawasiliano yanaendelea ili  ikisiri za makala haya ziweze kupatikana pia katika tovuti ya Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU).