“Korona wewe ni nani?” Uchambuzi Kilongo wa Ushairi kama Mkakati wa Kupambana na UVIKO-19

Authors

  • Angelus Mnenuka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Abstract

Miongoni mwa matukio makubwa yaliyoikumba dunia kuanzia mwaka 2020 ni mlipuko wa maradhi ya UVIKO-19. Kazi mbalimbali za sanaa zilitumiwa katika kuhamasisha kampeni ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu uliozua hofu kubwa duniani. Kwa kuwa kazi za sanaa huakisi ridhimu ya mawazo ya jamii, na kwamba wasanii ni zao la jamii, nyimbo nyingi za kuhamasisha vita dhidi ya UVIKO-19 zilisheheni mawazo yaliyotia hofu zaidi. Kinyume na matarajio ya wengi, Mrisho Mpoto alitumia mtindo tofauti. Badala ya kuendelea kuitia hofu jamii ili ifuate taratibu za kujikinga kama walivyofanya wengine, yeye aliitia jamii ujasiri na kuhamasisha kuondoa woga katika mapambano dhidi ya UVIKO-19. Katika makala haya, wimbo mmoja umeteuliwa kati ya nyimbo 25 kutokana na upekee wa mtindo uliotumiwa kuwasilisha maudhui yenye kuhamasisha mapambano dhidi ya UVIKO-19. Makala haya yametumia mkabala wa elimumitindo kuchambua mtindo wa wimbo wa “Kwaheri Corona” kwa kutumia Nadharia ya Uchambuzi Kilongo kama ilivyoasisiwa na Norman Fairclough. Matokeo yanaonesha kuwa msanii alitumia mtindo wa majigambo na ushairi wa kivita kama mbinu ya kujenga ujasiri kwa kukidunisha kirusi cha Korona na kuikweza jamii ya Watanzania. Mtindo huo ulilenga kuondoa woga uliotanda katika jamii nzima wakati wa mapambano dhidi ya janga la UVIKO-19.

DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na44t1.2

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2025-06-30

Issue

Section

Articles