Uchunguzi wa Ufundishaji wa Stadi za Kusoma na Kuandika katika Utekelezaji wa Mtaala Egemeo Uwezo nchini Rwanda

Authors

Abstract

Ufundishaji mwafaka wa stadi za kusoma na kuandika ni msingi wa kufanikisha Mtaala Egemeo Uwezo (kuanzia sasa MEU) katika somo la Kiswahili. Stadi hizi zinawawezesha wanafunzi kutumia Kiswahili katika mawasiliano rasmi na yasiyo rasmi, na kufanikisha shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinazohitaji matumizi ya Kiswahili. Makala haya yanalenga kuchunguza namna ufundishaji wa stadi za kusoma na kuandika unavyofanyika ili kutekeleza MEU. Makala pia yamelenga kueleza changamoto za ufundishaji wa stadi za kusoma na kuandika katika shule za sekondari za wilaya ya Nyamagabe, Rwanda. Mbinu za usaili, ushuhudiaji na uchambuzi wa matini zimetumika ili kukusanya data za kitaamuli, ambazo zimechambuliwa kimaelezo kwa kuongozwa na Nadharia ya Utamadunijamii ya Vygotsky. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa walimu wanatumia mbinu za ufundishaji ambazo haziwashirikishi wanafunzi kukuza stadi za kusoma na kuandika kwa ufanisi. Baadhi ya changamoto zilizobainika ni ukosefu wa vifaa vya kufundishia na wanafunzi kutokuwa na utamaduni wa kusoma. Hivyo, makala yamependekeza njia za kufanikisha ufundishaji wa stadi za kusoma na kuandika. Mapendekezo hayo ni kutumia kazi za andaa – shiriki - tafakari, na usomaji na uandishi changizi.

DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na44t1.6

 

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2025-06-30

Issue

Section

Articles