Matumizi ya Anagramu, Kanuni ya Rebasi, Seti, Emoji na Akronimi kama Mitindo ya Sanaa ya Uandishi

Benard Odoyo Okal

Abstract


Ikisiri Sanaa ya uandishi imeendelea kutokea katika mfumo wa kikabari, kihiroglifu, kilogografu, kisilabi, na kialfabeti. Imebainika kuwa tunapoendelea kimaandishi kutoka mfumo mmoja tunaelekea kuhama pia na vipashio vingine vya mifumo ya awali. Hivyo basi, chembechembe za mifumo ya awali zingali zinadhihirika katika mitindo mingine ya kisasa ya matumizi ya lugha kama tunavyoona katika rebasi, seti, na emoji. Kwa hiyo, makala haya yanalenga kufafanua mitindo ya rebasi, seti na emoji, pamoja na anagramu na akronimi kama sanaa ya uandishi ili kutambua ishara zinazotumiwa na zilizokubaliwa katika lugha. Makala yanahusisha dhana, dhima, historia, na maendeleo ya sanaa ya uandishi. Yanaonyesha pia jinsi mitindo ya anagramu, rebasi, seti, emoji, na akronimi inavyodhihirika kama sanaa ya uandishi. Data zilikusanywa maktabani kwa kutumia upekuzi, kuteuliwa kidhamirifu na kuchanganuliwa kimaudhui.

 

Dhana za msingi: uandishi, anagramu, rebasi, seti, emoji na akronimi


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.


 [ISSN 0856-9965 (Print)]