Ushairi wa Abdilatif Abdalla katika Kubainisha Utamaduni wa Waswahili

Authors

  • Joseph Nyehita Maitaria Chuo Kikuu cha Karatina
  • Richard Makhanu Wafula Chuo Kikuu cha Kenyatta

Abstract

Ikisiri

Makala haya yanafafanua maudhui yaliyomo katika tungo za mashairi ya Abdilatif Abdalla kwa kuzingatia namna masuala ya utamaduni waWaswahili yanavyowasilishwa. Masuala hayo yanahusu namna wenyeji hao wanavyotangamana na wanavyoshughulikia maisha yao kwa ujumla. Kadhalika, ubainishaji wa vipengele hivyo vimewasilishwa kwa kuzingatia taijriba ya mtunzi kama mmoja katika jamii hiyo. Mashairi hayo yanapozingatiwa, inabainika kuwa; hisi za mtunzi zimedhibitiwa kwa lugha teule ya mafumbo inayojikita katika zaidi katika ' lugha ' au ' lafudhi ' yake ambayo ni lahaja ya Kimvita. Katika muktadha huu, jumbe hizo zinahitaji fasiri na maelezo kutokana na utamaduni wa mtunzi. Kwa mapana, mashairi hayo yana mwangwi unaogusia historia yataifa lake (hasa katika miaka ya baada ya 1963 nchini Kenya). Kwa maana hii, ushairi wa Abdilatif Abdalla unaweza kwa kihifadhi na kibainishaji cha vielelelzo vya utamaduni na uhalisi wa maisha ya jamii ya mtunzi. Katika kushughulikia uhusiano uliopo kati ya fasihi na utamaduni, makala haya yanaangazia baadhi ya mifano ya mashairi yaliyohifadhiwa katika Diwani ya Sauti ya Dhiki (1973). Mwishowe, inapependekeza namna mashari teule ya Kiswahili yanavyoweza kuwa hifadhi ya ' viashiria ' vya ' viishara ' vyatamaduni asilia katika jamii ya sasa.

 

Abstract

This paper examines the poetry of Abdilatif Abdalla to determine the way in which social cultural issues of the Swahili people are presented. The issues relate to the way in which the people integrate and deal with their life affairs. In addition, the identification of the social cultural issues is based on how the poet, as a member of Swahili society, deals with them. The results show that figurative language, especially the Kimvita dialect, is used to hide the poet ' s feelings. Therefore, the poet ' s culture needs to be taken into account in the effort to unravel his messages. Generally, his poetry mirrors the history of his nation (since the years after Kenya ' s independence in 1963). Thus, the poetry of Abdilatif Abdalla can be a treasure trove of the culture and life of his people. In examining the relationship between literature and culture, this paper analyzes some of the poems in the anthology entitled "Diwani ya Sauti ya Dhiki" (1973). Finally, it makes recommendations  as to how peoms written in Kiswahili can preserve the people ' s real culture in the present society.

 

Dhana msingi: mashairi, Abdilatif Abdalla, utamaduni, Waswahili, mtunzi, lugha, uhalisi, viashiria, viishara

References

Abdalla, A. (1973). Sauti ya Dhiki.Nairobi: Oxford University Press.

Abdulaziz, M. H. (1979). Muyaka 19th Century Swahili Poetry:

Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Chacha, C. N. (1992). Ushairi wa Abdilatif Abdalla: Sauti ya Utetezi. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.

Imbosa, R. (1990). Jazanda katika Ushairi wa Muyaka. Tasnifu ya

Uzamili, Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).

Khatib, M. S. (1999). Tamathali za Usemi. MULIKA Juzuu, 25. Dar

es Salaam: TUKI.

Maitaria, J. N. (2014). Dhima ya Ushairi wa Kiswahili katika

Kuelimishia jamii kuhusu Demokrasia. KISWAHILI Juzuu, 77. Dar es Salaam: TATAKI.

Maitaria, J. N. (2017). Ushairi kama Chombo cha Kuhifadhia na

Kuelimishia Jamii kuhusu Utamaduni: Mfano wa Mashairi

Yanayotumia Methali. Katika M. Kandagor, N. Ogechi & C.

Vieke (wah.). Lugha na Fasihi katika Karne ya Ishirini na

Moja. Eldoret: Moi University Press.

Maitaria, J. N. (2018). Ushairi wa Muyaka kama Chombo cha

Kubainishia Historia ya Waswahilii. Katika Mwita, L. C. na Wenzake (wah.). Isimu na Fasihi ya Lugha za Kiafrika. Eldoret: Moi University Press.

Masinde, E. (2003). Ushairi wa Kiswahili na Maendeleo na

Mabadiliko ya Maudhui. Tasnifu ya Uzamivu, Chuo Kikuu

Cha Kenyatta. (Haijachapishwa)

Mbaabu, I. (1985). Utamaduni wa Waswahili.Nairobi: Publishing

and Book Marketing.

Momanyi, C. (1998). Usawiri wa Mwanamke Muislamu katika Jamii

ya Waswahili kama Inavyobainika katika Ushairi wa Kiswahili. Tasnifu ya Uzamili, Chuo kikuu Cha Kenyatta. (Haijachapishwa)

Mulokozi, M. M. (1999). Tanzu Tatu za Kale. Dar es Salaam: TUKI.

Mutonya, M. (2013). The Politics of Everyday Life in Gikuyu Popular Music in Kenya. Nairobi: Twaweza Communications.

Nassir, A. (1976). Malenga wa Mvita. Nairobi: Oxford Unversity

Press.

Njogu, K. & Chimerah, R. (1990). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia

na Mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Njogu, K. (1993). Dialogic Poetry: Contestation and Social Challenge in East African Poetic Genres. Tasnifu ya Uzamili, Chuo

Kikuu cha Yale. (Haijachapishwa).

Njogu, K. (2004). Reading Poetry as Dialogue. Nairobi: The Jomo

Kenyatta Foundation.

Nyanchama, M. B. (2004). Matumizi ya Taswira na Istiara katika

Sauti ya Dhiki. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).

Olsen, H. S. (1978). The Structure of Literary Understanding.

Cambridge: Cambridge University Press.

Senkoro, F. E. M. K. (1988). Ushairi: Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.

Shitemi, N. L. (2010). Ushairi wa Kiswahili Kabla ya Karne ya

Ishirini. Eldoret: Moi University Press.

Wafula, R. M. (2014). Nadharia za Uhakiki Kama Mchakato wa

Kutaalamisha Usomaji wa Fasihi. Journal of Linguistics and

Language in Education.

Wamitila, K. W. (2001). Kamusi ya Methali za Kiswahili. Nairobi:

Longhorn

Published

2019-03-13