Ubadilishaji Msimbo kama Mbinu ya Ukwezaji wa Staha Bungeni

Johanes Sylivester Balige

Abstract


Makala hii inalenga kubainisha jinsi ubadilishaji msimbo unavyotumika katika mijadala ya Bunge la Tanzania kama mbinu ya ukwezaji wa staha. Data za makala hii zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa nyaraka na ushuhudiaji. Uchambuzi na ufasiri wa data umetumia mkabala wa uchanganuzi kilongo, yaani kufasiri data kwa kuzingatia muktadha wa mazungumzo. Muktadha huo unajumuisha utu, sifa na hadhi ya msikilizaji, kanuni za kitaasisi na kijamii zinazodhibiti majadiliano, mahali pa mazungumzo, urasimi na mada ya mazungumzo. Data za makala hii zinaonesha kuwa ubadilishaji msimbo ni mbinu ya kistaha inayomwezesha mzungumzaji kulinda utu wa viongozi wakuu wa nchi, kupunguza mchomo wa kauli za matusi na kupunguza mchomo wa kauli zinazozungumzia mambo yanayohusu kujamiiana. Hali hii humwezesha mzungumzaji kuepuka kukiuka makatazo ya kijamii na kitaasisi yanayodhibiti mienendo isiyokubalika na hivyo kukweza staha.


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.