Usuli
Kioo cha Lugha ni jarida lililokuwa likitolewa na Chama cha Kiswahili cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya udhamini wa iliyokuwa Idara ya Kiswahili ya Chuo hicho. Uchapishaji wake ulikoma baada ya kufifia kwa chama hicho. Hali hii ilisababisha pengo la kitaaluma kwa kuwa majarida ya Kiswahili na Mulika hayakutosha kuchapisha makala zote zilizohusu taaluma ya Kiswahili. Matokeo yake, kuanzia mwaka 1995 Idara ya Kiswahili ililifufua jarida hilo na kuanza kulichapisha kama ‘Kioo cha Lugha Mfululizo Mpya’. Kuanzia mwaka 2009 jarida linachapishwa na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili baada ya Idara ya Kiswahili na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili kuungana. Hapo awali, makala zote zilikuwa zikiandikwa kwa Kiswahili lakini ili kupanua hadhira ya wasomaji na waandishi wa makala jarida linapokea miswada iliyoandikwa kwa Kiswahili na Kiingereza. Kwa sasa jarida ni mojawapo ya majarida ya kimataifa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambayo yanafanya vizuri sana.
ISSN 0856-552 X (nakala ngumu) & ISSN 2546-2210 (mtandaoni)