Role of Indigenous Languages in the Development of County Governments in Kenya
Abstract
Makala hii inahakiki nafasi ya lugha za asili katika maendeleo ya Serikali za Kaunti nchini Kenya. Kaunti nane ziliteuliwa katika utafiti huu; nazo ni Meru, Bomet, Kericho, Nakuru, Baringo, Uasin Gishu, Nandi na Bungoma. Aidha, makala imebainisha kielelezo cha matumizi ya lugha kama zana ya maendeleo, hasa kwa kujikita katika kaunti teule. Hatimaye, katika makala hii tumefafanua manufaa na madhara ya kutumia lugha za asili katika maendeleo ya Serikali za Kaunti zilizoteuliwa.