Lugha Ishara katika Dhifa za Jikoni (Kitchen Party) Nchini Tanzania

Authors

  • Doroth F. Mosha University of Dar es salaam

Abstract

Makala hii inahusu lugha ishara katika dhifa za jikoni nchini Tanzania. Makala imejikita zaidi katika kuzibaini na kuzifasiri lugha ishara na namna zinavyojidhihirisha kitamathali hasa zile zinazoundwa kisitiari na kitashibiha. Wafundaji katika dhifa za jikoni huwa na mbinu bunifu za kuunda ishara hizo na imebainika kuwa vifaa vya upambaji na baadhi ya zawadi zitolewazo kwa mwari huashiria maana fulani kimuktadha.   Dhifa za jikoni ni uwanda ambao unahitaji kuchimbwa kwa kina kitaaluma na kiutafiti kutokana na umuhimu wake katika maisha ya jamii hususani maisha ya ndoa. Dhifa za jikoni zimeibuka kutokana na tofauti zilizopo za maisha ya ndoa kati ya mume na mke na hata jamii na jamii. Benokraitis (2008) ana maoni kuwa taratibu za ndoa zinatofautiana baina ya jamii moja na nyingine kwa sababu wanajamii wa kila jamii hujijengea utamaduni unaoeleza kaida ambazo zinafafanua dhana ya ndoa. Data za makala hii zilikusanywa kwa kuhudhuria dhifa mbalimbali za jikoni jijini Dar es Salaam kwa kutumia mbinu ya ushuhudiaji wa ushiriki. Baadhi ya data zimechukuliwa katika tasnifu ya mtafiti. Uchambuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Mwitikio wa Wasomaji/Wasikilizaji.

Author Biography

Doroth F. Mosha, University of Dar es salaam

Mwandishi

Downloads

Published

2018-03-05

Issue

Section

Articles