Upinduzi wa Kimahali katika Lugha ya Kiswahili

Authors

  • Fabiola Hassan University of Dar es salaam

Abstract

Makala hii inahusu upinduzi wa kimahali katika lugha ya Kiswahili. Lengo lake ni kubainisha aina za upinduzi wa kimahali, vitenzi vinavyoruhusu na vile visivyoruhusu utokeaji wa mchakato huo, pamoja na vimahali vinavyoweza na vile visivyoweza kupinduliwa katika tungo. Data zimekusanywa kwa mbinu ya upitiaji wa nyaraka na usaili. Ufafanuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Sarufi Leksia Amilifu (SLA) ya Bresnan na Kaplan mwishoni mwa miaka ya 1970. Makala inabainisha kwamba, tofauti na lugha nyingine za Kibantu kama vile Kichewa (N31, Malawi) au Kizulu (S40, Afrika ya Kusini) ambazo zina upinduzi wa kimahali wa kimofolojia au wa kisemantiki, lugha ya Kiswahili ina aina mbili za upinduzi wa kimahali. Upinduzi huo hutokea iwapo muundo wa kitenzi kinachounda tungo una kithimu1 na kimahali2. Aidha, tofauti na lugha nyingine za Kibantu, kama vile Kiswana (S31, Botswana), katika lugha ya Kiswahili kitenzi ambacho muundo wake una mtenda hakiruhusu upinduzi wa kimahali. Vilevile, vimahali vinavyoweza kupinduliwa ni vijalizo. Kwa upande mwingine, vimahali visivyoweza kupinduliwa ni chagizo. Makala inahitimisha kwamba lugha ya Kiswahili inafanana na kutofautiana na lugha nyingine za Kibantu katika udhihirishaji wa upinduzi wa kimahali.
1.0

Downloads

Published

2016-02-13

Issue

Section

Articles