Mdhihiriko wa Kionjo cha Usangwini kwa Mhusika Willy Gamba katika Riwaya ya Njama

Authors

  • Athumani S. Ponera Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
  • Gervas A. Kasiga Chuo Kikuu cha Dodoma

Abstract

Maudhui ya kazi za kifasihi hufika kwa hadhira kupitia wahusika. Watunzi huwajenga wahusika hao kwa kutumia mbinu mbalimbali huku wakiwavisha haiba na mujukumu ambayo, aghalabu, huendana na vionjo maalumu vya haiba (psychological temperaments). Shabaha ya makala hii ni kufafanua namna ambavyo sifa na majukumu ya mhusika wa kazi za kifasihi huendana na vionjo vya kihaiba anavyojengwa navyo. Ufafanuzi wetu unaegemezwa kwenye uhusika wa Willy Gamba katika riwaya ya Njama. Tunaonesha namna anavyotekeleza majukumu yake kwa kuongozwa na sifa za kionjo cha usangwini ambacho ni mojawapo ya vionjo vikuu vinne vya kihaiba.

Author Biographies

Athumani S. Ponera, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Mwalim

Gervas A. Kasiga, Chuo Kikuu cha Dodoma

Mwalim

Downloads

Published

2020-02-17

Issue

Section

Articles