Hali ya Fasihi Simulizi ya Kiswahili katika Jamii ya Sasa na Mustakabali wake

Authors

  • Method Samwel Samwel Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam

Abstract

Makala hii inawasilisha hoja kuwa fasihi simulizi ni zao la jamii na kwamba inabadilika sambamba na mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni yanayotokea katika jamii. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia maandiko sita yahusuyo fasihi simulizi yaliyoandikwa katika vipindi mbalimbali. Maandiko hayo ni Finnegan  (1977), Mulokozi (1996 na 2017), Ngure (2003),  King ' ei na Kisovi  (2005) na Wamitila (2010). Maandiko haya yalituwezesha kutathmini fasihi simulizi inavyotazamwa katika vipindi mbalimbali na kuona mabadiliko katika dhana hiyo kulingana na mabadiliko ya jamii husika. Pia, data zilikusanywa kupitia utafiti wa uwandani. Data za uwandani zilikusanywa katika tanzu tatu ambazo ni ushairi simulizi, masimulizi na semi. Katika tanzu hizo tulitumia nyimbo za jadi na za kisasa, aina mbalimbali ya hadithi za kifasihi simulizi, na methali, vitendawili na misemo. Ilionekana ni muhimu kutumia tanzu mbalimbali ili kuonesha jinsi mabadiliko ya fasihi simulizi yanavyotokea. Uchambuzi na ufasiri wa data ulizingatia Nadharia ya Uhalisia, ambayo, zaidi ya mambo mengine, inabainisha kuwa kazi za fasihi husawiri maisha ya jamii husika (taz. Kearns, 1996; Ntarangwi, 2004). Uchambuzi wa data umebainisha kuwa tanzu mbalimbali za fasihi zimepitia mabadiliko mbalimbali na kwamba tanzu mpya zimeibuka na baadhi ya zamani zinaelekea kupotea.

Downloads

Published

2021-04-20

Issue

Section

Articles