Fonolojia Vipandesauti katika Lugha ya Kinyambo: Uzingativu wa Nadharia ya Fonolojia Leksika

Benitha France

Abstract


Makala hii inachunguza fonolojia vipandesauti katika lugha ya Kinyambo kwa kuzingatia Nadharia ya Fonolojia Leksika (FL). Data iliyochunguzwa ni sehemu ya data iliyokusanywa kutoka wilaya ya Karagwe mkoani Kagera. Nadharia ya FL, iliyoanzishwa na Kiparsky (1982) pamoja na Mohanan (1982), ndiyo imetumika katika uchambuzi wa data za makala hii. Nadharia hii inadhihirisha utegemeano wa fonolojia na mofolojia katika mchakato wa ujengaji neno, yaani mpangilio wa mizizi na viambishi katika neno hutawaliwa na kanuni za kifonolojia. Mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data ni hojaji na ushuhudiaji. Katika uchunguzi wa fonolojia vipandesauti katika Kinyambo, imebainika kuwa lugha hii ina utaratibu maalumu unaoonesha ni viambishi gani hutangulia kupachikwa kwenye mzizi wa neno na vipi hufuata na kwa utaratibu gani ambao una matokeo ya kifonolojia, yaani kanuni za kifonolojia zinatokea kila baada ya mchakato wa kimofolojia wa ujengaji neno ambapo kila umbo la nje la kimofolojia linazungukwa kupitia kanuni za kifonolojia kabla ya kiwango kinachofuata. Kwa hiyo, mifuatano ya viambishi katika maneno ya lugha hii husababisha kuathiriana kwa vipandesauti jirani, hivyo, kuibua mabadiliko mbalimbali ya kifonolojia ya vipandesauti hivi. Mabadiliko haya huhusisha kubadilika kwa sifa za kifonetiki za sauti inayohusika. Kwa hiyo, mahitaji ya kifonolojia yanaweza kubadili umbo la mofu ileile katika mazingira tofautitofauti kwa kutengeneza alomofu.


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.