Upitiaji Upya wa Michakato ya Kifonolojia na Kanuni zake katika Kiswahili Sanifu

Authors

  • Michael A. Mashauri Idara ya Lugha ya Kiswahili na Isimu, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Abstract

Makala hii inahusu upitiaji upya wa michakato ya kifonolojia katika Kiswahili sanifu huku ikizingatia matumizi ya Nadharia ya Fonolojia Zalishi. Michakato ya kifonolojia katika Kiswahili imeandikiwa na wataalamu wengi (taz. Maganga, 1992; Mgullu, 1999; Massamba na wenzake, 2004; Habwe na Karanja, 2004; Massamba, 2011; Obuchi na Mukhwana, 2015). Hata hivyo, bado kuna michakato mingine ambayo haijaguswa na wataalamu hawa na hata baadhi ya ile iliyoandikiwa haijafafanuliwa kwa kina kama vile ufifishaji wa irabu na usilabishaji. Aidha, kanuni za ujitokezaji wa baadhi ya michakato hiyo hazijaandikwa vizuri huku nyingine zikiwa hazijaandikwa kabisa. Vilevile, baadhi ya kanuni zilizoandikwa zina upungufu wa taarifa kiasi kwamba inakuwa vigumu kwa mjifunzaji kuelewa kwa urahisi mazingira ya utokeaji wa michakato inayohusika; mathalani, kanuni ya udondoshaji na ukaakaishaji. Makala hii inaijadili kwa kina michakato hiyo na kuandika kanuni kwa kila mchakato ili kuweka bayana mazingira ya utokeaji wa michakato hiyo. Aidha, makala imehusisha michakato yenye kutokana na mazingira ya kifonetiki na ile inayochombezwa na mazingira ya kimofolojia. Katika makala hii tunaiita kwa ujumla kama michakato ya kifonolojia.

Author Biography

Michael A. Mashauri, Idara ya Lugha ya Kiswahili na Isimu, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Mhadhiri

Downloads

Published

2022-04-18

Issue

Section

Articles