Athari za Kiimbo kwenye Maana za Kialami Pragmatiki ' mh ' katika Mazungumzo ya Kiswahili

Authors

  • Magreth J. Kibiki Idara ya Lugha na Fasihi, Kitivo cha Humanitia na Sayansi za Jamii, Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam

Abstract

Makala hii inahusu athari za kiimbo kwenye maana za Kialami Pragmatiki (kuanzia sasa KIPRA) mh katika mazungumzo ya Kiswahili. Data za makala hii zimekusanywa kutoka katika mazungumzo yasiyo rasmi yanayofanywa na wazungumzaji wa Kiswahili katika maeneo yasiyo rasmi kama vile kwenye vijiwe vya kahawa na vijiwe vya mamantilie. Uchambuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Umuktadhaishaji ya Gumperz (1982). Matokeo ya uchunguzi huu yanaonesha kwamba kiimbo kina uamilifu wa kubadilisha maana. Hii ni kwa sababu maana za KIPRA mh zinaonekana kubadilika kadiri KIPRA hicho kinavyosemwa kwa viimbo tofautitofauti. Miongoni mwa maana tulizozibaini katika makala hii ni kuashiria jibu la swali linalothibitisha jambo, kudokeza kwamba mzungumzaji anaanzisha mazungumzo, anashangaa jambo, anauliza swali linalomhamasisha mshiriki mwingine wa mazunguzo atoe jibu, kumtaka mshiriki mwingine wa mazungumzo arudie alichokisema au kuthibitisha zaidi kama kile alichokisikia ni sahihi au la, na kuonesha kuwa mzungumzaji amepatia jambo. Kwa ujumla, kiimbo kinaonekana kuwa na athari kwenye maana katika mazungumzo ya Kiswahili.

Author Biography

Magreth J. Kibiki, Idara ya Lugha na Fasihi, Kitivo cha Humanitia na Sayansi za Jamii, Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam

Mhadhiri

Downloads

Published

2022-04-18

Issue

Section

Articles