Usawiri Kijinsia wa Dhamira katika Misemo ya kwenye Vyombo vya Usafiri nchini Tanzania na Dhima zake kwa Jamii
Authors
Shani Omari Mchepange
Idara ya Fasihi, Mawasiliano na Uchapishaji, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaa
Abstract
Usawiri kijinsia ni mojawapo ya mada maarufu katika kazi za fasihi andishi na fasihi simulizi. Makala hii hailengi kuchunguza suala hili katika matini za kifasihi zilizozoeleka kuchunguzwa na watafiti mbalimbali kama vile riwaya, tamthilia, ushairi, hadithi na kadhalika. Lengo la makala hii ni kuchunguza usawiri wa kijinsia kupitia dhamira zinazopatikana katika misemo inayoandikwa katika vyombo vya usafiri nchini Tanzania. Eneo hili halijapewa aula miongoni mwa wahakiki wa fasihi ya Kiswahili wa masuala ya kijinsia. Data za makala hii zimekusanywa uwandani katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam kwa njia ya ushuhudiaji wa misemo iliyoandikwa katika vyombo hivi kama vile daladala, malori, bajaji, bodaboda na baiskeli. Aidha, data zilikusanywa kutoka katika matini andishi, tovuti, makundi ya kijamii kama vile WhatsApp na Facebook na usaili kwa baadhi ya madereva, makondakta na watumiaji wa vyombo hivi. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi Kilongo Tunduizi wa Kifeministi. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba misemo hii inasawiri masuala ya kijinsia kupitia dhamira mbalimbali kama vile mapenzi na ndoa, tabia na wajihi, uchumi na elimu. Usawiri huu kwa kiasi kikubwa unatweza jinsia moja na kukweza jinsia nyingine. Kutokana usawiri huo, mtazamo (wa jamii) kuhusu wanawake unapaswa kubadilika ili kuleta usawa wa kijinsia. Aidha, usawiri huu una dhima mbalimbali ikiwamo kuendeleza utamaduni wa jamii na kusawiri ukweli fulani wa maisha.
Author Biography
Shani Omari Mchepange, Idara ya Fasihi, Mawasiliano na Uchapishaji, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaa