Utoaji Majina ya Mifugo katika Gá´‰rá´‰mi: Uchunguzi wa Gá´‰irwana

Authors

  • Rehema Stephano Idara ya Kiswahili, Ndaki ya Insia na Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu cha Dodoma

Abstract

Makala hii inahusu uchunguzi wa utoaji wa majina ya mifugo katika lugha ya Gá´‰rá´‰mi, hususani katika lahaja ya Gá´‰irwana. Lengo kuu la makala hii ni kubainisha majina pamoja na vigezo vinavyotumika kutoa majina kwa mifugo katika jamii ya Gá´‰rá´‰mi. Utafiti uliozaa makala hii umetumia mbinu ya usaili katika kukusanya data, ambapo wafugaji kumi (10) wa jamii ya Gá´‰irwana kutoka kijiji cha Mpoku kilichopo wilaya ya Singida (Vijijini) walisailiwa. Matokeo yameonesha kuwa vigezo vikuu vinavyotumika katika utoaji wa majina ya mifugo katika Gá´‰rá´‰mi ni vinne ambavyo ni umri, ujinsi, rangi na dosari. Ng ' ombe huitwa kwa kutumia ujinsi na rangi, dosari (ulemavu), na umri na ujinsi. Mifugo mingine kama mbuzi, kondoo na kuku hutumia umri na ujinsi isipokuwa punda ambaye anatumia kigezo kimoja tu cha umri kwa sababu punda walio wengi wana rangi ya hudhurungi na wachache sana wana rangi nyeupe, na, aghalabu, matumizi makubwa ya punda ni kufanya kazi bila kujali jinsi. Aidha, matokeo ya utafiti yameonesha kuwa katika hatua ya kuzaliwa, mifugo mingi huwa na majina yanayofanana. Majina huanza kugawanywa kwa kuzingatia ujinsi katika hatua ya pili. Makala hii inapendekeza uchunguzi zaidi wa utoaji wa majina ya mifugo kuendelea kufanyika ili kuimarisha mawasiliano katika jamii mbalimbali za wafugaji na kuyahifadhi majina hayo kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Author Biography

Rehema Stephano, Idara ya Kiswahili, Ndaki ya Insia na Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu cha Dodoma

Mhadhiri Mwandamizi

Downloads

Published

2022-04-18

Issue

Section

Articles