Matumizi ya Sitiari katika Kazi za Fasihi: Mifano kutoka Nyimbo za Kivunjo

Authors

  • Ernesta S. Mosha University of Dar es salaam

Abstract

Makala hii inajadili matumizi ya sitiari kutoka katika nyimbo za Wachaga wa Vunjo. Kwa kuongozwa na Nadharia ya Mwingiliano (Black, 1962), makala imeweka bayana namna ambavyo sitiari katika kazi za fasihi zinatumika kuugawa, kuupanga na kuueleza ulimwengu. Kwa kutumia data kutoka katika nyimbo tatu za taasisi ya ndoa kutoka katika jamii ya Wachaga wa Vunjo, makala imebainisha kuwa watunzi wa kazi za fasihi huunda sitiari kutoka katika mazingira na maisha halisi ya jamii ambayo wahusika wameyazoea. Pia, sitiari hizo hubuniwa kutoka katika mazingira mahususi ya kiutamaduni hali ambayo inalazimu ufafanuzi wake kuzingatia utamaduni na mazingira husika ili iweze kueleweka. Aidha, imebainika kuwa kupitia sitiari zilizotumika katika nyimbo teule, wanajamii wanafahamishwa namna ya kukabiliana na hali mbalimbali wanazokutana nazo katika maisha. Kwa njia hii, fasihi ina nafasi kubwa ya kubuni mbinu zinazoweza kuleta mabadiliko kwa wanajamii kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.

Author Biography

Ernesta S. Mosha, University of Dar es salaam

Mhadhiri

Downloads

Published

2023-05-17

Issue

Section

Articles