Ubainikaji wa Aina za Ukatili wa Watoto katika Fasihi ya Kiswahili ya Watoto: Mifano kutoka Riwaya Teule

Enock N. Nyariki, Pamela Ngugi

Abstract


Makala hii imeangazia aina za ukatili wa watoto katika riwaya za Siku Njema (Walibora, 1996), Tumaini (Momanyi, 2006) na Lulu ya Maisha (Habwe, 2013) ambazo zinalenga hadhira ya watoto na vijana. Wachambuzi wengi wa fasihi ya Kiswahili ya watoto wamemwangazia mtoto kama mwathiriwa wa matendo ya ukatili. Kipengele cha mtoto kama mhusika katili ambaye matendo yake yanaweza kuwaathiri wanajamii wengine hakijahakikiwa kwa kina. Katika misingi hii makala iliangazia aina za matendo ya ukatili wa watoto katika vitabu teule vya fasihi ya watoto. Nadharia ya Uhalisia ambayo waasisi wake ni pamoja na Gustav Flaubert (1850), Rene Wellek (1963) na Lazaro Carreter (1970) ilitumika ili kuonesha jinsi ukatili wa watoto ulivyoakisiwa na waandishi. Data za msingi zilipatikana kwa kusoma vitabu teule. Aidha, makala ilinufaishwa kwa kuzisoma na kuzihakiki kazi zinazohusiana na mada hii kwenye majarida, magazeti, tasnifu, vitabu na machapisho mbalimbali. Maelezo ya kina yalitumiwa kuwasilisha matokeo ya utafiti. Aina tatu za ukatili zilijitokeza katika riwaya. Aina hizo ni ukatili wa kimatendo unaojibainisha katika matendo kama vile uvamizi, wizi na unyang’anyi; ukatili wa kimatamshi, ambao hubainika katika vitisho na matamshi ya kudhalilisha; na ukatili wa kifikra, ambao hujidhihirisha kwa ishara za maandishi, matamshi na kuwaandamaandama waathiriwa kwa nia ya kuwadhuru.


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.