Changamoto katika Matumizi ya Majina ya Lugha za Kigeni nchini Tanzania: Mtazamo wa Nadharia ya Ubeberu wa Kiisimu

Authors

  • Adventina Buberwa Idara ya Lugha ya Kiswahili na Isimu, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Abstract

Wataalamu mbalimbali wameshughulikia suala la uteuzi wa majina ya watu ndani na nje ya Tanzania. Baadhi ya wataalamu (taz. Nyangaywa, 2013; Madila, 2020) wanaeleza kwamba uteuzi wa majina ya watu nchini Tanzania unakabiliwa na changamoto ya kasumba ya kupendelea majina ya lugha za kigeni kuliko majina ya lugha za asili. Pamoja na kudokezwa kwa suala hilo, tafiti husika hazikujishughulisha na uchunguzi zaidi kuhusu kuweka bayana kiwango cha matumizi ya majina husika na changamoto zinazotokana na matumizi ya majina hayo ya kigeni. Suala hili limechochea raghba ya mtafiti kufanya utafiti wa awali kuhusu kiwango cha matumizi ya majina ya lugha za kigeni katika jamii ya Watanzania, mtazamo wa jamii na changamoto zinazotokana na matumizi ya majina hayo nchini Tanzania. Ili kutimiza azma hiyo, makala hii imeongozwa na Nadharia ya Ubeberu wa Kiisimu ambapo kasumba hiyo ya kupendelea majina ya lugha za kigeni inatazamwa kama matokeo ya lugha za kigeni kukandamiza lugha za asili na kutokana na ukandamizaji huo, fikra za jamii ya Watanzania zimeaminishwa kuwa lugha za kigeni ni bora na zina thamani zaidi kuliko lugha za asili.

Author Biography

Adventina Buberwa, Idara ya Lugha ya Kiswahili na Isimu, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Mhadhiri Mwandamizi,

Downloads

Published

2023-05-17

Issue

Section

Articles