Tathmini ya Matumizi na Kukubalika kwa Istilahi za Simu kwa Wazungumzaji wa Kiswahili Nchini Tanzania

Authors

  • Majura Nyangaywa University of Dar es sa
  • Pendo S Malangwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Abstract

Makala hii inaangazia hali ya matumizi na kukubalika kwa istilahi za Kiswahili za simu za mkononi miongoni mwa wazungumzaji wa Kiswahili nchini Tanzania. Data zilikusanywa kwa mbinu ya usomaji matini, hojaji na usaili kutoka kwa watoataarifa katika kata za Kimara na Ubungo, Dar es Salaam. Nadharia ya Ulinganifu wa Kiathari ilitumika katika makala hii. Matokeo yanaonesha kuwa baadhi ya wazungumzaji wanakubali kutumia istilahi za Kiswahili za simu na wengine hawakubali. Aidha, makala inabainisha sababu mbalimbali zilizotolewa na kila upande. Makala inapendekeza kuwapo kwa ushirikishwaji wa wazungumzaji wa Kiswahili, wataalamu wa teknolojia ya mawasiliano na wataalamu wa istilahi wakati wa mchakato wa uundaji wa istilahi za Kiswahili za simu za mkononi.

Author Biographies

Majura Nyangaywa, University of Dar es sa

Mwalim

Pendo S Malangwa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Mwalim

Downloads

Published

2023-05-17

Issue

Section

Articles