Misingi ya Matumizi ya Wakaa katika Usimulizi wa Riwaya za Kiswahili: Mifano kutoka Nagona na Mzingile
Authors
Athumani S. Ponera
University of Dar es salaam
Jasmine Kinga
University of Dar es Salaam
Abstract
Makala hii inajadili kuhusu wakaa kama kipengele cha kibunilizi katika utunzi wa kazi za fasihi. Shabaha kuu ni kufafanua misingi iliyomwongoza mwandishi kutumia wakaa kwa jinsi inavyodhihirika katika kazi teule. Nadharia ya Umuundo imetumika kama kiunzi cha kukusanyia data pamoja na kuendeshea mjadala wa makala. Data za makala hii zilipatikana kwa kutumia njia ya udurusu wa nyaraka. Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa, ujenzi wa wakaa katika kazi teule umeegemea katika misingi ya kiutamaduni, kipokezi na kitajiriba.