Athari za Mabadiliko ya Maana katika Lugha ya Kiswahili: Mifano kutoka Matini za Kidini

Authors

  • Lydiah S Mwenje University of Dar es salaam
  • Stanley A Kevogo

Abstract

Makala hii inachanganua matumizi ya lugha katika mahubiri ya kidini. Azma kuu ni kuchunguza jinsi maana za maneno zinavyobadilika kiisimu zinapotumiwa kwenye miktadha ya mahubiri ya Kikristo. Data ya utafiti imetokana na unukuzi kimaandishi wa vipindi 5 vya mahubiri ya Kikristo yaliyorekodiwa kati ya Mei na Agosti, 2020 kutoka idhaa tatu za runinga nchini Kenya, yaani KBC, SAYARE na MBCI. Wahubiri 5 waliotumia Kiswahili tu kwenye vipindi vya idhaa hizi ndio walioteuliwa kwa usampulishaji kusudio. Data ya semi 64 zilizoteuliwa kwa usampulishaji huo zilichanganuliwa kwa mwongozo wa madhumuni ya utafiti pamoja na mihimili ya Nadharia ya Pragmatiki Leksika. Matokeo yanaonesha kwamba baadhi ya maneno yaliyotumiwa na wahubiri wa dini za Kikristo huwasilisha maana kipragmatiki. Maana za maneno hayo kimatumizi ni tofauti na maana msingi. Aidha, uchunguzi huu unaazimia kuendeleza mtazamo wa isimu kuhusu jinsi matumizi ya lugha katika muktadha wa sajili hii maalumu unavyoathiri mawasiliano.

https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v21i1.5

Author Biographies

Lydiah S Mwenje, University of Dar es salaam

MWALIM

Stanley A Kevogo

MWALIM

Downloads

Published

2024-01-22

Issue

Section

Articles