Nyimbo za Jando za Jamii ya Wagogo na Maudhui yake

Authors

  • Rose J Mbijima University of Dar es salaam

Abstract

Nyimbo za jando ni utanzu mmojawapo wa fasihi simulizi ya makabila mengi. Kabla ya ujio wa wageni asasi ya jando ilitazamwa kama chombo cha ujamiishaji na uhifadhi wa hekima na falsafa za jamii. Kupitia nyimbo za jando mafunzo mbalimbali yalitolewa kwa vijana na jamii kwa ujumla. Makala hii imechunguza nyimbo za jando za jamii ya Wagogo na kubainisha maudhui yanayojitokeza katika nyimbo hizo. Nadharia ya Sosholojia ya Fasihi iliyotumika katika utafiti huu imetuwezesha kuzikusanya na kuzichambua data za awali na za upili. Data za awali zimekusanywa katika tarafa ya Kongwa mkoani Dodoma kwa kutumia mbinu za mahojiano na ushuhudia. Data za upili zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya upitiaji nyaraka uliofanywa kwenye maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Makavazi ya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili. Utafiti huu umebaini kuwa nyimbo za jando za jamii ya Wagogo zina maudhui mbalimbali na ya msingi yakiwamo; umuhimu wa tohara kwa vijana, kuwaandaa vijana kumudu majukumu ya utu uzima, ujamiishaji na uadilishaji vijana. Mengine ni ukarimu, umoja na ushirikiano katika jamii, umuhimu wa kudumisha mila, desturi na utamaduni wa jamii na masuala ya kijinsia.

https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v21i1.10

Author Biography

Rose J Mbijima, University of Dar es salaam

Mwalim

Published

2024-01-22

Issue

Section

Articles