Yaliyomo

Kioo Cha Lugha

Abstract


Juzuu la 21 toleo la 1 lina jumla ya makala 10 zinazohusu mada mbalimbali za isimu na fasihi. Makala ya Shao na Kotira inahusu uainishaji wa ngeli za nomino za lugha ya Kivunjo kwa kutumia Nadharia ya Mofolojia Asilia na Mkabala wa Viambishi Awali vya Nomino. Nao Lomayani na Mgecha wamechunguza jinsi unyambulishaji unavyoathiri uelekezi wa vitenzi vya lugha ya Kimasai. Watafiti hao wametanabahisha kwamba unyambulishaji husababisha kuongezeka, kudondoshwa au kuhamishwa kwa yambwa katika vitenzi vya Kimasai. Makala ya Stephano inahusu ukarabati wa irabu katika lugha ya Girmi ili kuepuka mfuatano wa irabu zinazofanana katika mpaka wa kisintaksia. Aidha, utafiti wake umebainisha michakato ya kifonolojia inayotumiwa katika ukarabati huo wa irabu.

Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.