Matumizi ya Mandhari za Kifasihi Simulizi katika Ujenzi wa Dhamira za Ushairi Andishi: Mifano kutoka Diwani za Muhammed Seif Khatib

Authors

  • Baraka Sikuomba University of Dar es salaam
  • Joviet Bulaya

Abstract

Makala hii inakusudia kuchunguza jinsi mandhari za fasihi simulizi zilivyotumika kujenga dhamira katika diwani za Fungate ya Uhuru (1988), Wasakatonge (2003) na Vifaru Weusi (2016). Sababu ya uchunguzi huu ni kwamba mandhari ni kipengele muhimu cha fani katika ujenzi wa kazi za fasihi andishi kama vile riwaya, tamthiliya na hadithi fupi kuliko utanzu wa ushairi. Data za makala hii zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini. Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji iliyoasisiwa na Wolfgang Iser (1978), Stanley Fish (1980), James Tompkins (1980), Haus Robert Jauss (1982) na Robert Holub (1984) ndiyo iliyoongoza ukusanyaji na uchambuzi wa data za makala hii. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kuna matumizi ya mandhari za fasihi simulizi katika kujenga dhamira. Dhamira hizo ni matabaka, ushujaa na ujasiri, ukombozi wa kifikra, kutoheshimu taaluma na uzalendo wa kweli.

 

                                        DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v21i2.2

Downloads

Published

2024-04-08

Issue

Section

Articles