Mdhihiriko wa U-Naijeria katika Video za Nyimbo za Muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania

Gervas A Kasiga

Abstract


Makala hii inajadili mdhihiriko wa U-Naijeria katika video za nyimbo za muziki wa kizazi kipya wa Kiswahili nchini Tanzania. Utafiti wa makala hii uliendeshwa kitaamuli. Makala ilitumia usanifu wa kifenomenolojia, ambapo tafakuri ilikuwa ni kiini katika kuhusisha na kutoa majawabu ya taarifa mbalimbali zilizochunguzwa. Misingi ya Nadharia ya Uhalisia ilitumika katika ukusanyaji na uchambuzi wa data za utafiti wa makala. Katika uainishaji wa matokeo ya utafiti, mdhihiriko wa U-Naijeria katika video za nyimbo za muziki wa kizazi kipya wa Kiswahili nchini Tanzania ulibainika katika vipengele vya mavazi, ala na midundo ya muziki, mitindo ya kiuchezaji, mandhari, utumiwaji wa vifaa vya kijukwaa na matumizi ya lugha. Mwisho, imependekezwa kuwa ni muhimu kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya wa Kiswahili nchini Tanzania kuhusisha vipengele vya utamaduni katika uundaji wa video zao ili kuwezesha ukuzaji wa sanaa, mila, desturi na maadili ya Kitanzania.

 

                DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v21i2.3


Full Text:

218-232

Refbacks

  • There are currently no refbacks.