Uhawilishwaji wa Wakaa wa Kihehe na Athari zake katika Ujifunzaji wa Kiswahili Sanifu kama Lugha ya Pili

Authors

  • Ngenzi Ngenzi University of Dar es salaam

Abstract

Makala hii imechunguza uhawilishwaji wa wakaa wa Kihehe na athari zake katika ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya pili. Lengo kuu ni kuchunguza namna uhawilishwaji wa wakaa wa Kihehe katika lugha ya Kiswahili unavyoiathiri lugha hiyo. Data zilikusanywa kutoka kwa wajifunzaji wa lugha ya Kiswahili wa jamii ya Wahehe na walimu wa somo la Kiswahili kwa kutumia mbinu za masimulizi ya hadithi na usaili. Uchambuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Usasanyuzi Linganishi. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa uhawilishwaji wa wakaa wa Kihehe katika Kiswahili husababisha athari katika lugha hiyo. Athari iliyobainika ni mabadiliko ya matamshi ya maneno mbalimbali ya Kiswahili ambayo husababisha ubadilishaji wa maana msingi za maneno husika. Ili kuondoa au kupunguza athari hiyo, makala hii imependekeza uelimishaji wa jamii za vijijini kuhusu umuhimu wa lugha ya Kiswahili. Pia, serikali iandae walimu wa kutosha ambao ni wabobezi wa kufundisha Kiswahili kama lugha ya pili.

 

                              DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v21i2.7

Downloads

Published

2024-04-08

Issue

Section

Articles