Matumizi ya Fantasia katika Fasihi ya Kiswahili Yanavyoibua, Kujenga na Kuwasilisha Dhamira

Authors

  • Gerephace Mwangosi Chuo Kikuu Katoliki cha Mbeya

Abstract

Makala hii imechunguza namna kipengele cha fantasia katika fasihi ya Kiswahili kinavyoibua, kujenga na kuwasilisha dhamira. Lengo la makala hii ni kuchunguza namna kipengele cha fantasia kinavyotumika kuibua, kujenga na kuwasilisha dhamira katika riwaya ya Kiswahili. Data za msingi zilipatikana katika riwaya teule ya Kusadikika kwa mbinu ya usomaji makini. Nyaraka zilizotumika kufafanua na kuthibitisha data za msingi zilipatikana kwa mbinu ya kielektroniki na kimaktaba. Uchambuzi na mjadala wa data uliongozwa na Nadharia ya Semiotiki. Msingi mkuu wa nadharia hii ni kushughulika na ishara pamoja na uashiriaji katika kazi za fasihi. Matokeo ya utafiti yamewasilishwa kwa mbinu ya kimaelezo. Matokeo yameonesha namna msuko wa fantasia katika kitabu teule unaivyoibua dhamira zinazolenga kuifunza, kuiimarisha na kuiweka jamii pamoja katika misingi imara ya utamaduni, siasa na uchumi. Dhamira zilizoibuliwa zinawasilisha matendo ya msingi ya binadamu yanayojidhihirisha katika nyanja zote za maisha na maendeleo yake. Kwa hiyo, makala hii inapendekeza kuwa utafiti ufanyike zaidi katika tanzu za fasihi simulizi ya Kiswahili kuhusu matumizi ya fantasia yanavyofumbata masuala ya uchumi, siasa, utamaduni, falsafa na itikadi za jamii.

DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v22i1.7

Downloads

Published

2024-06-30