Mtindo wa Usambamba katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi

Authors

  • Aloo R. Odhiambo Chuo Kikuu cha Nairobi
  • Kineene wa Mutiso Chuo Kikuu cha Nairobi
  • Kyallo W. Wamitila Chuo Kikuu cha Nairobi

Abstract

Katika makala hii tumechunguza aina mbalimbali za usambamba na mchango wake katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi. Ili kufanikisha hili, makala imeongozwa na Nadharia ya Umitindo ambayo inachunguza na kutoa fasiri kwa kazi za isimu na fasihi. Nadharia hii imetumika katika makala hii kwa kuwa uchunguzi wa vipengele vya kifasihi hutegemea vile vya kiisimu. Nadharia ya Umitindo inahusishwa na Geoffrey Leech (1969) hasa katika andiko lake la A Linguistic Guide to English Poetry. Lengo la uhakiki wetu ni kuweka wazi aina mbalimbali za usambamba zinazobainika katika utenzi huu na michango yake katika kufanikisha fani na maudhui kwenye utungo huu. Kutokana na uchunguzi wetu, tumebainisha kuwa matumizi ya usambamba kama aina ya urudiaji yanachangia katika ukuzaji na uendelezaji wa dhamira, usawiri na ujenzi wa wahusika na kuingiliana na sifa nyingine za kimtindo ili kuibua umbuji wa kijumla wa utungo huu.

DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v22i1.8

Downloads

Published

2024-06-30