Mabadiliko ya Utambulisho wa Mwanamke na Uimarishaji wa Ujinsuke

Mifano kutoka Riwaya ya Nyuso za Mwanamke (Mohamed, 2010)

Authors

  • Ernesta S. Mosha Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Abstract

Tafiti mbalimbali kuhusu riwaya ya Kiswahili zinaonesha kuwa mwanamke amesawiriwa kwa mitazamo mbalimbali, ukiwamo mtazamo hasi. Usawiri wa mtazamo huo unamtambulisha mwanamke kama kiumbe dhaifu na duni. Kwa kuongozwa na Nadharia ya Udenguzi, makala imeonesha namna mhusika mwanamke anavyoweza kubadilisha utambulisho hasi na kujenga utambulisho chanya. Makala imetumia data kutoka katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke (Mohamed, 2010) zilizopatikana kwa usomaji makini. Makala imeweka bayana nafasi ya riwaya ya Kiswahili katika kujenga utambulisho wa mwanamke unaoimarisha ujinsuke. Matokeo haya yanatokana na uumbaji wa wahusika wanawake wanaodengua kaida za jamii zinazomkandamiza mwanamke na kufichua mbinu zinazotumiwa na baadhi ya wanajamii kuendeleza ukandamizaji huo. Pia, umuhimu wa wanawake kujitambua na kujisimamia umewekwa bayana.  

DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v22i2.3

 

 

Author Biography

Ernesta S. Mosha, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Mhadhiri Mwandamizi

Downloads

Published

2024-12-30