Tofauti za Kifonolojia na Kimsamiati baina ya Kiswahili cha Kigoma, Ujiji na Kiswahili Sanifu

Authors

  • Ahmad Y. Sovu Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam

Abstract

Watanzania wengi, hususani waishio vijijini, wana lugha zao za asili ambapo hujifunza Kiswahili na kukitumia kama lugha ya pili. Watanzania hao, wanapotumia Kiswahili huonekana wakibadili baadhi ya sauti na maneno. Makala hii inalenga kuchunguza tofauti za kifonolojia na kimsamiati baina ya Kiswahili cha Kigoma Ujiji na Kiswahili sanifu ili kubaini tofauti za matumizi ya sauti na maneno kati ya lugha hizo. Data zimekusanywa kwa kutumia ushuhudiaji na majadiliano ya vikundi. Uchambuzi na uwasilishaji wa data umeongozwa na Mkabala wa Mbinu Linganishi (Anttila, 1972). Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa kuna tofauti ya kifonolojia baina Kiswahili cha Kigoma, Ujiji na Kiswahili sanifu katika sauti zenye maneno yenye asili ya kigeni kama vile sauti [h], [bu], [mu]. Pia, kuna tofauti ya mabadiliko ya sauti [a] badala ya sauti [ha], [s] kuwa [sh], [r] badala ya [l], [bh] badala ya [b] na [bu] au [tu] kuwa [wa]. Aidha, kuna tofauti za matumizi ya sauti [-ga], lafudhi na mabadiliko ya kialami [ngo] badala ya sauti [eti] na tofauti za urefushaji irabu. Katika muktadha huo, Kiswahili cha Kigoma, Ujiji kinafanana na kutofautiana na Kiswahili sanifu kifonolojia na kimsamiati. Hata hivyo, tofauti zilizobainika ni zile za ubadilishaji wa sauti na msamiati usio wa msingi katika lugha hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinatokana na athari za lugha mama.

DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v22i2.4

Author Biography

Ahmad Y. Sovu, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam

Mhadhiri

Downloads

Published

2024-12-30