Uchanganyaji Msimbo katika Jamiilugha za Mitandaopepe

Mtagusano wa Kiswahili na Kiingereza

Authors

  • Rhoda P. Kidami Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Abstract

Mitandaopepe imetoa fursa kwa watu kutagusana katika masuala anuwai ya kijamii. Kiswahili ni miongoni mwa lugha zinazotumiwa katika mitandaopepe, ndani na nje ya Tanzania. Kutokana na kukua na kusambaa kwa lugha hiyo ulimwenguni kote, kuna haja ya kuchunguza mwonekano wake katika muktadha huo wa kimawasilianopepe. Lengo la makala hii ni kuchunguza jinsi Kiswahili kinavyotagusana na lugha ya Kiingereza katika mawasiliano hayo, hususani kwenye kipengele cha uchanganyaji msimbo. Data za utafiti huu ni maoni yaliyotolewa kwenye mtandao wa YouTube baada ya watu kusikiliza hotuba za Kiswahili za Mwalimu Nyerere. Jumla ya maoni elfu mbili na sitini yalikusanywa kutoka katika hotuba tatu. Uchanganuzi wa data hizo uliongozwa na Kiolezo cha Myers-Scotton (2001) kinachohusu lugha msingi na lugha changiaji katika kipengele cha uchanganyaji msimbo. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kwamba lugha za Kiswahili na Kiingereza zinakamilishana katika muktadha wa kimawasilianopepe. Katika miktadha tofautitofauti, lugha mojawapo imetumiwa kuwa msingi wa mawasiliano huku nyingine ikijaliza sarufi ya lugha msingi. Wakati mwingine, lugha zote mbili zimetumiwa kwa pamoja huku kila moja ikijikamilisha kisarufi.

DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v22i2.5

Author Biography

Rhoda P. Kidami, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Mhadhiri Mwandamizi

Downloads

Published

2024-12-30