Mwelekeo wa Usarufishaji wa Nomino za Kiswahili zenye Asili ya Kiingereza na Kiarabu

Authors

  • Johari Hakimu Chuo Kikuu Mzumbe, Tanzania

Abstract

Makala hii inaonesha mwelekeo wa usarufishaji wa nomino za Kiswahili zenye asili ya Kiingereza na Kiarabu. Mwelekeo wa nomimo hizo umeoneshwa kwa kutumia data iliyokusanywa kwa njia ya upitiaji wa nyaraka. Nyaraka zilizopitiwa ni Kamusi Kuu ya Kiswahili (2022) na Kamusi ya Karne ya 21 (2021). Data iliyopatikana ilichanganuliwa kwa kutumia Nadharia ya Mofolojia ya Ongezeko la Maneno na kufafanuliwa kwa kutumia Nadharia ya Usarufishaji. Uchanganuzi na ufafanuzi wa data hizo umeonesha kuwa kuna mielekeo chanya na hasi ya usarufishaji wa nomino za Kiswahili kwa kuzingatia ngeli za majina. Mwelekeo chanya wa usarufishaji wa nomino za Kiswahili zenye asili ya Kiingereza na Kiarabu umeonesha mchakato wa usarufishaji uliokamilika katika Kiswahili. Mwelekeo hasi umedhihirisha usarufishaji usiokamilika katika baadhi ya nomino za Kiswahili zenye asili ya Kiingereza na Kiarabu. Kwa ujumla, ufafanuzi wa nomino za Kiswahili unapaswa kuzingatia mazingira ya namna zinavyojitokeza na kusarufishwa katika lugha hii.

DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v22i2.6

 

Author Biography

Johari Hakimu, Chuo Kikuu Mzumbe, Tanzania

Mhadhiri

Downloads

Published

2024-12-30