Ubabedume katika Ushairi wa Kiswahili: Mfano wa Utenzi wa Fumo Liyongo

Authors

  • John M Kobia
  • Rose Mung ' ahu

Abstract

Suala la uana limepewa kipaumbele miongoni mwa masuala yanayotafitiwa katika taaluma mbalimbali zinazohusu maisha ya binadamu. Majukumu ya jinsi ya kike na jinsi ya kiume ni suala ambalo linaendelea kuzua mgogoro miongoni mwa watu wa jamii mbalimbali. Hata hivyo, utafiti wa uana unaozingatia jinsi ya kiume katika Kiswahili, hususan fasihi simulizi haujashughulikiwa kwa kina. Tafiti nyingi zilizopo zimeshughulikia masuala ya kike. Kuna haja ya utafiti kufanywa kuhusu suala la jinsi ya kiume katika fasihi, hususan katika ushairi wa jadi wa Kiswahili. Makala haya yanachunguza suala la ubabedume katika Utenzi wa Fumo Liyongo kwa kuzingatia majukumu, sifa na nafasi ya mwanamume katika utenzi huu. Makala yameongozwa wa nadharia ya ubabedume inayosisitiza maumbo ya vitambulishi vya jinsia ya kiume kwa kuzingatia jamii, maandishi na matukio au maelezo ya kihistoria.

 

Downloads

Published

2017-08-22

Issue

Section

Articles