Unyambulishaji na Dhana ya Uelekezi katika Lugha ya Kikuria

Authors

  • Mary Z Charwi

Abstract

Mofolojia ya vitenzi ni uwanja muhimu katika lugha yoyote ile duniani kutokana na ukweli kuwa kila lugha ina vitenzi na tabia ya vitenzi hutofautiana kutoka lugha moja hadi nyingine. Vitenzi vya lugha za Kibantu vina sifa ya kuambikwa viambishi awali na viambishi tamati. Mojawapo ya viambishi tamati ni viambishi vya kauli mbalimbali. Viambishi hivi huweza kuathiri muundo wa kitenzi ama muundo wa tungo kwa ujumla katika kuleta maana inayohusika. Mfano, kitenzi elekezi huweza kuwa si elekezi, si elekezi huweza kuwa elekezi ama kitenzi elekezi kuhitaji yambwa nyingine. Makala haya yanalenga kuelezea matokeo ya vitenzi vya Kikuria baada ya unyambulishaji na idadi ya viambishi vinavyoweza kuwekwa pamoja kwenye kitenzi.

Downloads

Published

2017-08-22

Issue

Section

Articles