Mikinzano ya Kimtazamo baina ya Wahusika Inavyobainisha Falsafa ya Kiafrika

Mifano kutoka Riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo (2007)

Authors

  • Winne S. Mtega Mhadhiri

Abstract

Tofauti za kimtazamo baina ya wahusika zimekuwa zikijitokeza katika kazi mbalimbali za riwaya. Watunzi wa kazi hizo wamekuwa na kawaida ya kuwavisha wahusika uhusika unaopambanua mawazo, imani, itikadi na falsafa mbalimbali zinazoongoza maisha yao. Kuwapo kwa mitazamo hiyo, kumechochea tafiti nyingi kuchunguza falsafa ya waandishi wa kazi hizo, mitazamo ya wahusika na uhusika wao na Uafrikanishaji wa kazi hizo, hususani za riwaya. Makala hii inalenga kuchunguza mikinzano ya kimtazamo baina ya wahusika na namna inavyobainisha falsafa ya Kiafrika. Data za utafiti zimepatikana uwandani kupitia njia ya usomaji na uchambuzi matini. Mchakato wa uchambuzi umeongozwa na Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa mikinzano ya kimtazamo baina ya wahusika katika riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo (2007) imejitokeza katika masuala ya ndoa, uzazi, malezi, utamaduni na ujamaa. Vipengele hivyo ndivyo vimeibua mikinzano ya kimtazamo baina ya wahusika na kubainisha falsafa ya Kiafrika kwamba maisha ya Mwafrika yamejengwa katika kuthamini uzazi kama mhimili wa kuwapo na mwendelezo hai wa vizazi.

DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v23i1.5

Author Biography

Winne S. Mtega, Mhadhiri

Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu, Mkwawa, Iringa, Tanzania

Downloads

Published

2025-06-30