Mbinu za Ujenzi wa Masuala ya Kiuhalisia Hakiki na Dhima zake katika Riwaya za Kichwamaji (1974) na Dunia Uwanja wa Fujo (1975)

Authors

  • Tusingwire Timon Mhadhiri Msaidizi
  • Leonard F. Ilomo Mhadhiri,

Abstract

Mtindo wa uhalisia hakiki unahusu uandishi wa kazi za fasihi ambapo masuala anuwai ya kijamii hubainishwa na mwandishi pasipo hofu yoyote. Mwandishi anapotumia mtindo huu katika uandishi wake huchambua maovu yaliyopo kwenye jamii na kuyaweka wazi bila kificho chochote. Wakati mwingine, uandishi wa namna hii huhatarisha usalama wake. Hivyo, ni waandishi wachache sana wenye uthubutu huo hasa kama maovu hayo yanawahusu wenye mamlaka moja kwa moja. Makala hii imechunguza mbinu zinazotumika kujenga masuala ya kiuhalisia hakiki katika uandishi pamoja na dhima za mtindo huo katika riwaya za Kichwamaji (1974) na Dunia Uwanja wa Fujo (1975) zilizoandikwa na Euphrase Kezilahabi. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini wa matini teule. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Uhalisia kwa kujikita katika mkabala wake wa uhalisia hakiki. Matokeo yameonesha kwamba kuna mbinu tano zinazotumika kujenga masuala ya kiuhalisia hakiki kiuandishi ambayo ni majadiliano baina ya wahusika, matendo ya wahusika, uzungumzinafsiya, sitiari na uwasilishaji dhahiri. Kwa upande mwingine, dhima za mtindo huo ni kumpambanua msanii, kumtafakarisha msomaji, kujenga jamii mpya na kuibua mambo mapya katika jamii.

DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v23i1.6

Author Biographies

Tusingwire Timon, Mhadhiri Msaidizi

Taasisi ya Taaluma za Lugha, Chuo Kikuu cha Kabale, Uganda

Leonard F. Ilomo, Mhadhiri,

Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania

Downloads

Published

2025-06-30