Ufahamu wa Wanachuo Kuhusu Akili-Unde katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili, Tanzania
Abstract
Utafiti huu umejikita kuchunguza ufahamu wa wanachuo juu ya akili-unde katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili. Wanachuo 30 wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam wamehusishwa katika upatikanaji wa data za utafiti huu. Data zimechanganuliwa kwa mbinu ya uchambuzi wa dhamira ya mkabala wa kitaamuli. Imebainika kuwa wanachuo wengi wana uelewa wa akili-unde na wanaitumia katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili. Wamekiri kwamba wanapotumia akili-unde kujifunza lugha ya Kiswahili wanakumbana na changamoto kama vile upataji wa maudhui usio sahihi, mapungufu katika kutafsiri sarufi ya lugha ya Kiswahili, matatizo ya kiufundi na hofu. Ili kutatua changamoto hizo za akili-unde katika tathmini ya ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili wanachuo wametaja zana zinazoweza kutumika. Zana hizo ni pamoja na hojaji, ushuhudiaji, mitihani na majaribio. Japo baadhi ya zana hizo zinasisitiza kukariri maudhui na siyo kujifunza kwa vitendo, bado wahadhiri wanaweza kutengeneza maswali tunduizi yanayokuza umahiri. Matokeo haya yanasisitiza umuhimu wa kufanyika tafiti zaidi kuhusu programu za akili-unde zinazotumika kujifunza na ubora wa maudhui yanayopakuliwa kupitia akili-unde. Hii itapunguza wasiwasi uliopo juu ya matumizi ya akili- unde katika ufundishaji, ujifunzaji na tathmini ya lugha ya Kiswahili katika elimu ya juu.
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright © by Department of Foreign Languages and Linguistics, University of Dar es Salaam
All rights reserved. No part of this publication may be reproduced or transmitted in any form or by any means, electronic or mechanical, including photocopying, recording, or any information storage or retrieval system, without permission in writing from the publisher, except for short extracts in fair dealing, for research or private study, critical scholarly review or discourse with an acknowledgement.