Uambatanishaji katika Lugha ya Kiswahili

Authors

  • Luinasia Elikunda Kombe University of Dar es Salaam, Dar es Salaam

Abstract

Makala hii inahusu uambatanishaji katika lugha yaKiswahili. Lengo ni kuonesha upekee wa lugha ya Kiswahili katika uambatanishaji ili kubaini ufanano na utofauti uliopo baina ya lugha ya Kiswahili na lugha nyingine. Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika makala hii kuonesha upekee huo ni aina za uambatanishaji katika lugha ya Kiswahili, aina za viunganishi ambatanishi, idadi na mtawanyo wa viunganishi ambatanishi katika tungo ambatani na namna viunganishi ambatanishi vinavyotofautiana kulingana na aina na idadi ya viambatanishwa. Data za makala hii ni za utafiti wangu wa uzamivu zilizokusanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa matini. Uchanganuzi wa data hizo katika makala hii umeongozwa na Nadharia Msingi ya Isimu. Matokeo yanabainisha kuwa, Kiswahili kina aina mbili za uambatanishaji, yaani uambatanishaji kwa kiunganishi dhahiri na uambatanishaji bila kiunganishi dhahiri. Pia, imebainika kuwa lugha ya Kiswahili ina aina mbalimbali za viunganishi ambatanishi na ni lugha inayotumia kiunganishi kimoja katika kuunganisha viambatanishwa viwili. Halikadhalika, imebainika kwamba viunganishi ambatanishi vya Kiswahili hutofautiana kimatumizi kwani vipo vinavyoambatanisha virai na vishazi na vinavyoambatanisha vishazi pekee. Pia, imebainika kwamba kuna vinavyoambatanisha viambatanishwa viwili tu na vinavyoambatanisha viambatanishwa zaidi ya viwili.

Author Biography

Luinasia Elikunda Kombe, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam

Department of Languages and Literature, Dar es Salaam University College of
Education.

Published

2025-09-11