Ujumuishaji wa Tafakuri Tunduizi katika Mitihani ya Taifa ya Shule za Sekondari Nchini Rwanda: Mfano wa Kiswahili Kidato cha Sita
Abstract
Tafakuri tunduizi inawawezesha wanafunzi wa lugha kufanya kazi kwa ufanisi kuzidi wanafunzi wengine ambao hawakuikuza. Hii inatokana na kwamba wanafunzi wenye stadi hii huwa na uwezo wa kufikiri kihakiki kuhusu masuala yanayohusiana na mazingira ya kazi na maisha kwa ujumla. Pamoja na hayo, fasihi inachukuliwa kama nyenzo ya kukuza stadi za tafakuri tunduizi kutokana na uchangamano wa vipengele vyake. Hivyo basi, makala yetu inalenga kujadili ujumuishaji wa stadi za tafakuri tunduizi katika mitihani ya Kiswahili ya taifa kwa shule za sekondari nchini Rwanda. Kupitia uchambuzi wa mitihani ya taifa ya somo la Kiswahili na matini mbalimbali kuhusu tathmini ya tafakuri tunduizi, tumebaini kwamba stadi za tafakuri tunduizi hazijumuishwi kwa ufanisi katika mitihani ya taifa ya somo la Kiswahili hasa katika kipengele cha fasihi. Baadhi ya maswali ya mtihani hayawapi wanafunzi uhuru wa kuhusisha hali ya darasani na maisha halisi ya utatuzi wa matatizo. Kwa hivyo, makala imetoa mikakati inayopaswa kuzingatiwa ili kuandaa maswali ya mitihani ya lugha ya Kiswahili kwa kujumuisha tafakuri tunduizi ipasavyo. Baadhi ya mikakati hiyo ni pamoja na kuzingatia malengo na mahitaji ya mwanafunzi na yale ya mtaala tumizi, kuhakikisha kuwa mwanafunzi anapewa fursa ya kuzalisha mawazo mapya kama matokeo ya ujifunzaji na kuandaa maswali ya mtihani yanayoakisi mazingira halisi ya utatuzi wa matatizo.
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright © by Department of Foreign Languages and Linguistics, University of Dar es Salaam
All rights reserved. No part of this publication may be reproduced or transmitted in any form or by any means, electronic or mechanical, including photocopying, recording, or any information storage or retrieval system, without permission in writing from the publisher, except for short extracts in fair dealing, for research or private study, critical scholarly review or discourse with an acknowledgement.