Changamoto za Wanafunzi Wanaojifunza Lugha ya Kichina kama Somo kwa Wajifunzaji Wanaotumia Kiswahil Kama Lugha ya Kwanza katika Kumudu Stadi za Lugha: Mifano kutoka Shule Teule za Sekondari Nchini Tanzania

Authors

  • Rabiel Shabani Fadhil University of Dar Es Salaam

Abstract

Kichina ni lugha mojawapo kati ya lugha za kigeni zinazofundishwa katika
shule za sekondari nchini Tanzania. Katika kuboresha zoezi zima la
ujifunzaji na ufundishaji wa somo la kichina katika shule za sekondari,
makala hii imelenga kubainisha changamoto zinazokwamisha wanafunzi
kuwa mahiri na namna bora ya kuweza kukabiliana na changamoto hizo.
Utafiti huu uliwahusisha walimu na wajifunzaji katika shule za sekondari
zinazofundisha kichina katika mkoa wa Dodoma, halmashauri ya jiji la
Dodoma. Shule ya sekondari Umonga, Dodoma na Kiwanja cha Ndege
zilihusishwa katika utafiti huu. Aidha, mbinu za mahojiano, uchambuzi
matini na ushuhudiaji zilitumika kupata data za utafiti huu. Mkabala wa
kitaamuli uliongoza uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Matokeo ya utafiti
huu yanatarajiwa kuwasaidia watunga sera na wadau mbalimbali wa elimu,
kuongoza uboreshaji wa ufundishaji wa lugha na utoaji wa rasilimali.
Kimsingi matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa zipo changamoto
zinazokwamisha umahiri wa wajifunzaji wa Kichina kama lugha ya pili
kama vile ; tofauti za kiisimu baina ya Kichina na Kiswahili, walimu
kutokuwa mahiri katika lugha wanayofundisha, suala la mazingira finyu ya
kujifunzia na upungufu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Pia, utafiti
huu utachangia katika mjadala mpana wa kitaaluma kuhusu elimu ya lugha
za kigeni barani Afrika, na kupendekeza njia za uchunguzi wa siku zijazo.

Author Biography

Rabiel Shabani Fadhil, University of Dar Es Salaam

Department of Languages and Literature

Assistant Lecturer

Published

2024-12-09