DHIMA YA USHAIRI WA KISWAHILI KATIKA KUELIMISHIA JAMII KUHUSU DEMOKRASIA

Authors

  • Joseph Nyehita Maitaria University of Dar es salaam

Abstract

 

Makala haya yanafafanua dhima ya Ushairi wa Kiswahili katika kubainisha na kuielimishia jamii kuhusu masuala ya demokrasia. Ushairi kama kitengo muhimu cha fasihi, umekuwa ukitumiwa kuchochea usaili na tafakari kuhusu uhusika wa watu katika uongozi wa jamii. Aidha, umaarufu wake hautokani tu na maneno ya lugha iliyozoewa katika jamii bali kupitia kwa tamathali za usemi ambazo huhusishwa kwa makusudi katika ubebaji wa ujumbe unaowasilishwa.Hivyo, utanzu huu unakuwa ni nyenzo ya kuwaelekeza, kuwaelimisha na kuwazindua watu kuhusu uwajibikaji wa kushiriki na kuchangia kwa dhati katika masuala ya siasa na uongozi wa jamii. Katika miaka ya mwanzo mwanzo mwa 1960 hadi miaka ya 1990, serikali za mataifa ya Afrika Mashariki zimekuwa zikijitahidi kwa kiwango fulani lakini hazijaudhibiti mwafaka wa kuhusisha umma katika masuala muhimu ya kitaifa. Kutokana na mabadiliko asasi za jamii ya sasa, kumekuwa na mitazamo tofauti tofauti kuhusu falsafa na matarajio ya watu kuhusu uelekezaji wa maisha yao. Baadhi ya wanajamii wamekuwa wakisaili na kukemea baadhi ya vitendo hasi vinavyoshuhudiwa katika mfumo wa utawala uliopo katika jamii. Kadhalika, ushairi wa Kiswahili umekuwa ukiyabainisha na kuyafakari baadhi ya masuala hayo kwa jicho pekuzi. Kwa maana hii, suala la demokrasia linashughulikiwa katika makala haya kwa kurejelea baadhi ya mashairi ya Abdilatif Abdalla, Sauti ya Dhiki (1973), Alamin Mazrui, Chembe cha Moyo (1988) na Said Ahmed Mohammed, Jicho la Ndani (2002).

Author Biography

Joseph Nyehita Maitaria, University of Dar es salaam

Mwandishi

Downloads

Published

2017-10-03

Issue

Section

Articles